Noah Henry: Hadithi ya Upinde wa Mvua

Noah Henry anaambiwa kwamba hataweza kucheza na rafiki zake kwa sababu ya korona. Lakini, wakati Noah na familia yake wanapoondoka kwenda matembezini, anatambua ya kwamba hivi karibuni, mambo yatarudi kuwa mazuri.

  • Langues disponibles :

 

  • UKRAINIEN
  • HEBREU
  • GREC
  • ROUMAIN

12.99

500 en stock

Description

Kama siku yoyote nyingine, Noah Henry anajitayarisha kwenda shuleni-lakini, wazazi wake wanamwambia kwamba shule yake imefungwa. Zaidi ya hilo, bustani ya wanyama pia imefungwa na hataweza kucheza na rafiki zake wanaoishi mle. Mambo hayabadiliki hata wakati Noah na kaka yake mdogo wananawisha mikono yao kama walivyoambiwa na walimu wao. Lakini, wakati Noah na familia yake wanapoondoka kwenda matembezini, anagundua ya kwamba rafiki zake walikuwa wamechora pinde za mvua na kuziweka kwenye madirisha yao, na anatambua ya kwamba rafiki zake pia hawana hakika kuhusu siku zijazo, na ya kwamba siku moja yeye na rafiki zake watacheza pamoja tena.

About the Author

Deana Sobel Lederman ni mwandishi na mchoraji. Bibi yake alikuwa mchoraji ambaye alisomea kwenye chuo kiitwacho
The Art Students League of New York. Alimfundisha Deana kuhusu uchoraji wakati Deana alikuwa mchanga sana, na mamake Deana pia alimhimiza kuchora kutoka wakati Deana alikuwa mchanga. Deana alichora kitabu chake cha kwanza cha ucheshi kinachoitwa The Wacky Couples wakati alikuwa na miaka minane, na baadaye alikuwa mchoraji mkuu wa gazeti la wanafunzi wa UC Berkeley na msanii aliyechapishwa. Baadaye, alisomea kuhusu sheria ya hakimiliki kwenye chuo kikuu cha sheria. Ameishi New York City; Berkeley, California; London, England; na Cambridge, Massachusetts. Deana alikulia katika mji wa San Diego, California, na hapo ndipo anapoishi pamoja na mume wake na watoto wake wawili.

Informations complémentaires

Poids 0.093 kg
To Be Read Books

1

Avis

Il n’y a pas encore d’avis.

Soyez le premier à laisser votre avis sur “Noah Henry: Hadithi ya Upinde wa Mvua”

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *